Kiswahili
HIGHLANDS HOPE CONSORTIUM
….bringing patient-focus,high-quality,sustainable HIV-AIDS treatment to rural Africa
Highland Hope Consortium(HH) ni mtandao wa hospitali tatu zinazojiendesha kwa kujitegemea(binafsi)nyanda za juu kusinimwa Tanzania. Mbili kati ya hizo ziko chini ya mhimili ya kidini na tatu ipo chini ya kampuni ya TANWAT Njombe.
Zote kwa pamoja zinawajibika katika mapambano dhidi ugonjwa UKIMWI kwa miongo kadhaa ndani ya vijiji na vya Tanzania na rasilimali zake. Wajibu wao umetawaliwa na mtazamo ulio wazi katika kutimiza mahitaji ya wagonjwa katika kuweka usawa na umakini ukilinganisha na upungufu /ukosefu rasilimali za huduma za Afya ili kuwezesha huduma zenye uhakika kutolewa katika maeneo hayo
Jumuiya ya Hospitali za HH ni mojawapo ya vitengo nyeti vyenye kutoa huduma ya afya nchini Tanzania vyenye mipango iliyo thabiti katika kutoa huduma. Ya ushauri nasaha na kupima,kugawa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa ya UKIMWI pamoja na huduma za ufuatiliaji wa afya ya. Wagonjwa hospitalini na majumbani.
HIGHLANDS HOPE HOSPITALS
Hospitali za Highlands Hope zinaendeleza kwa vitendo mipango ya matibabu ya virusi vya UKIMWI katika maeneo ya vijiji vya Afrika. Kufuatia kauli mbiu ya idara ya Taifa ya kupambana na ugonjwa wa UKIMWI (NAPC) ukilinganisha na rasilimali hafifuya huduma za afya za wagonjwa kwenye maeneo ya vijijini,hivyo kuandaa mikakati halisi na zana zitakiwazoili kuweka mipango hii katika utekelezaji Ulio thabiti.
Maendeleo ya njia za kupambana/kuzuia na kuangalia matokeo ya kazi ndio shabaha kuu ya HH.katika makubaliano kati ya washiriki mama na muungano wa karibu na NAPC, HH inahamisha matumizi ya sayansi na teknolojia pamoja na uvumbuzi katika kuhakikisha kwamba huduma bora zinaendelezwa siku zote kulenga ubora wa huduma kwa wagonjwa na utedaji wake.
HIGHLANDS HOPE TEAM AND PARTNERS
Highlands hope ni mjumuiko wa watu waliobobea katika masuala ya kutoa huduma za afya,Elimu kwa jamii,pamoja na kujitolea kufanya kazi na mamia ya wtu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika wilaya Maketena Njombe Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.(bofya kitufe cha NEWS katika menu kusoma zaidi kuhusu kazi zao na mafanikio)
Hospitali za HH zinafanya kazi na jamii za maeneo ya vijijini;wajumbe wa makanisa ikiwa ni pamoja na Romani katoliki Dayosisi ya Njombe pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali mfano MSF ambalo linapatikana katika mkoa wetu.

Print this Page
Bookmark this Page
